NALA_Money_Squarespace_Lead_Visual_1280x720_1-03.jpg

Njia rahisi zaidi na salama ya kufanya miamala Tanzania na Uganda

 
 

Miamala. Kirahisi. Haraka.

 

NALA inakuwekea huduma za kifedha kwenye mikono yako. Hamna tena mchakato mrefu wa USSD *150*xx#.

 
 
Ninaweza kuona salio za akaunti zangu zote mbili katika programu moja, NALA inarahisisha shughuli zangu za miamala.
— Hamisi Masunga, Mwanza, Tanzania
Ukiachana na muonekano wake mzuri, kitu kikubwa kuhusu NALA ni kwamba ni rahisi sana kutumia.
— Enock Mbise , Tanga, Tanzania
Sidhani kama nimeshawahi kutumia programu yenye manufaa hapa Tanzania kama programu ya NALA.
— Emmanuel Massawe, Moshi, Tanzania
Timu yangu kazini huwa wanatumia NALA. Kila siku ni kama wanashindana kuangalia nani katuma pesa kwa haraka zaidi. NALA ipo vizuri!
— Oliver Masaua, Dar es Salaam, Tanzania

Tunalinda familia ya NALA. Hii ndio jinsi tunavyofanya hivyo: 

NALA_Money_Squarespace_Security_400x720_1-01.jpg

Ulinzi wenye hadhi ya kibenki

NALA inatumia mfumo wa usalama unaotumika na mabenki 500 kubwa duniani, na imethibitishwa na washirika wetu wa kimataifa.

Uthibitishaji wenye vipengele mbalimbali

NALA inawapatia watumiaji wake uwezo wa kutengeneza PIN ya NALA kwa ulinzi wa ziada juu ya PIN yako ya mobile money.

Ulinzi wa taarifa

Ukikamilisha muamala kwa kutumia NALA, PIN yako ya mobile money (tiGO, Vodacom au Airtel) hulindwa na mtandao wako. NALA haihifadhi PIN zozote.

Ukaguzi wa akaunti

Timu ya NALA mara kwa mara huwa tunakagua kazi zetu, ujumbe wetu, na akaunti zetu ili kuhakikisha usalama wa mteja.

Imethibitishwa na mitambo ya Google

NALA inatumia mitambo iliyothibitishwa na Google kwa kila muamala.

Familia inalinda familia. Je, bado una swali kuhusu usalama wa NALA? Tuandikie kwenye security@nala.money