Pata Kuijua NALA

NALA ni nini?

NALA ni programu(App) ya kufanya miamala yako kwa urahisi, uharaka na kwa usalama zaidi bila kutumia Internet. NALA inakuwezesha kutuma pesa, kutoa pesa, kulipia bili mbalimbali, kununua vifurushi, kufanya manunuzi, kujua na kufuatilia historia ya matumizi yako kwa urahisi bila ya kuongeza gharama yoyote.

Je, ninahitaji akaunti ya benki ili niweze kutumia NALA??

Hapana, NALA haihitaji akaunti ya benki, ili uweze kutumia NALA Unatakiwa uwe una akaunti na mitandao ya simu.

Kwa nini tulianzisha NALA?

NALA Inc. Inaamini ya kuwa kuna ulazima wa kutengeneza Mfumo Jumuishi wa kiuchumi na kifedha unaohusisha na kuboresha maisha ya kila mtu. Soma Makala hii kutoka kwa Muanzilishi wa NALA kuhusu sababu za kuanzisha NALA

Ni watu gani wanaounda familia ya NALA?

Ukipakua application ya NALA unakuwa umejiunga kwenye Familia yetu inayoamini katika mifumo inayosaidia kujenga jamii yetu kwa pamoja.

Je, ninaweza kutumia NALA kwenye iPhone?

Kwa sasa, NALA inapaikana kwenye simu zenye za Android tuu kwenye Google Playstore. NALA haifanyi kazi kwenye iOS.

NALA itanigharimu shilingi ngapi kutumia? Je, kuna ada za matumizi?

Kutumia NALA ni Bure, Hakuna Ada za Matumizi wala gharama za nyongeza.

Mama NALA ni nani?

Mama NALA ni msaidizi wako kutoka familia yetu ya NALA. Yupo kwa ajili ya kujibu maswali yoyote kuhusu NALA. Tunajenga NALA kwa pamoja na tunathamini sana maoni yako.

Vipengele vya NALA

Ninaipataje App ya NALA?

Kwasasa NALA Inapatikana kwenye Google Playstore.

Ni mitandao gani ya simu niwezayo kutumia na Nala?

Airtel, Halotel, tiGO, TTCL, Vodacom na Zantel.

Ninaweza kutumia NALA kama sina intaneti/data?

Ndiyo. NALA inakamilisha Miamala yako yote bila ya kuunganishwa na intaneti

Ninaweza nikatuma pesa kwa mtu asiyekuwa na app ya NALA?

Ndiyo, unaweza ukatuma pesa kwa watu wote wenye laini za mitandao inayofanya miamala. Sio lazima wawe watumiaji wa NALA.

Ninaweza nikatumia app ya NALA nisipokuwa na salio kwenye simu?

Ndiyo, unaweza ukakamilisha miamala yoyote hata bila salio kwenye simu.

Nikiwa natumia NALA kutuma pesa, ni PIN gani ninayotumia?

Ukiwa unafanya muamala , weka PIN (yaani namba ya siri) ya Akaunti yako. PIN ya NALA ni kwaajili ya kufungulia app yako tu.

Kwa nini ninaona gharama ninapo fanya shuguli kwenye programu ya NALA?

Hizo ni gharama (Ada) zile zile za mitandao yako ya simu zinazotozwa ukifanya miamala yako hata bila App ya NALA. Unaweza ukaangalia gharama hizo hapa

  1. Vodacom
  2. tiGO
  3. Airtel Money
  4. Halotel
  5. Zantel
  6. TTCL

Usalama

Nina uhakika gani kwamba ni salama kutumia NALA?

NALA inatumia ULINZI wenye hadhi ya kibenki kwa kuhakikisha ya kuwa taarifa zako na miamala unayofanya ipo salama. Kwa maelezo zaidi tafadhali soma www.nala.money/usalama

PIN yangu ya NALA ni sawa na PIN yangu ya muamala wa pesa(mobile money)?

PIN yako na NALA sio lazima ifanane na PIN yako ya Muamala wa Pesa(Mobile Money).Chaguo la PIN ni lako, lakini tunashauri kuwa na PIN mbili tofauti kati ya NALA na Miamala wa Pesa(Mobile Money) kwa kuwa ni salama zaidi.

Je, NALA inahifadhi Namba zangu za siri?

Hapana, NALA haihifadhi namba zako za siri. NALA inatumia teknolojia ile ile inayoaminiwa na kutumiwa na makampuni makubwa ya Visa na MasterCard.

Je, Simu yangu ikiibiwa, watu wengine wanaweza wakahamisha pesa kutoka kwenye App yangu ya NALA?

Kulinda akaunti yako dhidi ya uhalifu au wizi tunashauri uunde PIN ya NALA . Hamna atakayeweza kutumia akaunti yako kufanya miamala kama hawafamu PIN yako ya NALA na ya miamala.

Ujumbe mfupi kuhusu Miamala

Nini kitatokea niki tuma pesa kwa bahati mbaya, na nitawezaje kurejeshewa pesa zangu?

Tafadhali, piga simu kwa mtandao wako na uwajulishe kwamba umetuma hela kwa bahati mbaya. Watakusaidia kwa tatizo lako.

Nitajuaje hali ya Malipo niliyofanya?

Programu ya NALA itakuambia kama muamala umekamilika au kama umeshindikana. Pia unaweza ukapata thibitisho kupitia njia ya SMS kutoka kwa mtandao wa simu unayotumia.

Kwanini baadhi ya shuguli zangu hazitambuliki kuwa zimekamilishwa katika historia ya miamala?

Huduma za kutuma pesa na kulipia bili ndizo zinazoonekana kwenye historia ya miamala. Hamna historia ya manunuzi ya vifurushi. Shughuli zilizositishwa nazo hazioneshwi kwenye historia ya miamala.

Nini kitatokea nisipo pokea SMS kutoka M-Pesa, tiGO Pesa au Airtel Money inayothibitisha shuguli niliyofanya?

Kwa kawaida ,tatizo kama hili huwa halitokei, lakini likitokea tafadhali wajulishe Vodacom, tiGO au Airtel kwa msaada.

MMI Error ina maana gani?

MMI Error ina maana kuna Tatizo kwenye upande wa mtandao wako na hii ni nje ya uwezo wa NALA. Unaweza ukajaribu kuwasha na kuzima simu yako au unaweza ukasubiri mtandao ujirekebishe baada ya muda kidogo.